Kila mwaka, changamoto ya wanafunzi kuchelewa kukamilisha assignment inaendelea kuonekana katika shule, vyuo na hata kwa wanafunzi wa kujisomea. Lakini je, nini hasa kinachowafanya washindwe kumaliza kwa wakati?
1. Kukosa Uongozi wa Muda (Poor Time Management)
Wanafunzi wengi hawajui kupanga majukumu yao kwa kipaumbele.
Kuchelewesha (procrastination)
Kufanya mambo dakika za mwisho
Kutokua na ratiba ya kujisomea
2. Kutokuelewa Somo au Maelekezo
Baadhi ya wanafunzi hushindwa kuanza kazi mapema kwa sababu hawajui wanatakiwa kufanya nini hasa.
Maelekezo magumu
Uoga wa kuuliza
Kukosa rasilimali zinazoweza kusaidia
3. Msongo wa Mawazo na Majukumu Mengi
Wanafunzi wengi wanabeba majukumu mengine nje ya masomo.
Kazi za nyumbani
Majukumu ya kifamilia
Kazi ndogo za kujipatia kipato
4. Kutokua na Motivation ya Kusoma
Motisha ndogo husababisha mwanafunzi kukosa nguvu ya kuanza.
Kutoona faida ya assignment
Kutokuwa na malengo ya muda mrefu
Kutovutiwa na somo husika
5. Changamoto za Teknolojia
Kwa baadhi, vifaa na mtandao ni tatizo.
Kukosa laptop/smartphone
ntaneti duni au ghali
Kushindwa kutafuta taarifa mtandaoni
6. Muda Mdogo Kwa Kazi Kubwa
Wakati mwingine tatizo si mwanafunzi, bali mzigo wa kazi.
Walimu kutoa assignment nyingi kwa wakati mmoja
Muda uliopewa kutokuwa rafiki
Hitimisho
Ili wanafunzi waongeze kasi ya kumaliza assignment kwa wakati, wanahitaji ratiba nzuri, maelekezo rahisi, mazingira rafiki ya kujisomea, na msaada wa walimu. Pia ni muhimu kuacha tabia ya ku
fanya kazi dakika za mwisho na kujenga nidhamu ya kusoma kwa utaratibu.
ChuoSmart Notifications